Niungeni mkono 2017 uwe mwaka wa amani duniani- Guterres
Katika Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye anaanza kazi rasmi hii leo, ametaka dunia kuungana naye katika kusaka suluhu ya matatizo lukuki yanayoikabili sayari hiyo.
Guterres ambaye leo ni anaanza rasmi jukumu lake hilo, amesema hayo katika wito wake wa amani kwa jumuiya ya kimataifa akisema mwaka wa 2017 uwe wenye nuru na utatuzi akisisitiza.
( Sauti Guterres)
“Katika siku hii ya mwaka mpya, nawasihi nyote muungane nami kuweka azimio la pamoja la mwaka mpya: Hebu na tuazimie kuweka mbele amani. Hebu na tuufanye mwaka 2017, uwe mwaka ambao kwao sisi sote, raia, serikali, viongozi tunahangaika kumaliza tofauti zetu.
Kuhusu madhila ya vita na athari zake Katibu Mkuu amesema hakuna mshindi zaidi ya mateso kwa raia.
( Sauti Guterres)
“Makombora mazito yanaangukia raia. Wanawake, watoto na wanaume wanauawa na wanajeruhiwa, wakilazimika kukimbia makwao, bila mali zao na kusalia hohehahe. Hata hospitali na misafara inalengwa.”
Guterres kadhalika amezungumzia umuhimu wa mshikamano katika kufikia suluhu.
( Sauti Guterres)
“Kuanzia mshikamano na upendo kwenye maisha yetu ya kila siku hadi mazungumzo na kuheshimiana katika migawanyiko yetu ya kisiasa….Kuanzia kusitisha mapigano kwenye maeneo ya vita hadi kulegeza misimamo kwenye meza za mazungumzo na kufikia suluhu ya kisiasa.Amani lazima iwe lengo na mwongozo wetu.”