Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya tabinachi na hatua za kukabiliana nazo huko nchini Tanzania

Mabadiliko ya tabinachi na hatua za kukabiliana nazo huko nchini Tanzania

Jarida letu maalum leo linaangazia athari za mabadiliko ya tabinachi na hatua za kukabiliana nazo huko nchini Tanzania.

Mwezi Novemba mwaka jana nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi walikusanyikka mjini Marrakech nchini Morocco, kwa ajili ya mkutano wa 22 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP22.

Mkutano huo ulimalizika kwa tamko lilioitwa "enzi mpya ya utekelezaji na hatua kuhusu mabadiliko ya tabia nchi." Tamko la kuchochea hatua madhubuti za kuhakikisha kiwango cha joto kinasalia nyuzi joto mbili katika vipimo vya Celsius na hatua nyingine anuai.

Wakati wa mkutano huo Benki ya dunia iliwasilisha ripoti inayoonyesha kuwa nchi za Afrika zinafanya vyema katika jitihada za kukabaliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Ripoti hiyo imezisifu nchi kama vile Cote d'Ivoire na Nigeria kwa juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hususani katika kupunguza hewa ya ukaa. Benki ya dunia ilipitisha mpango maalum wa usaidizi kwa nchi zinazoendelea katika kutimiza jukumu hilo muhimu baada ya kuanza kutekelezwa kwa mkataba wa  Paris wa mabadiliko ya tabianchi mwaka uliopita wa 2016.

Nchini Tanzania, athari za mabadiliko ya tabiachi zinaonekana  katika nyanja kadhaa ikiwemo kuongezeka kwa kina cha bahari hatua inayohatarisha kumezwa kwa nchi kavu.

Kufahamu  kwa undani tuungane na Martha James wa redio washirika Pangani Fm ya Tanga, anayeangazia hatua zinazochukuliwa katika kukabiliana na mabadiliko hayo wilayani Pangani