Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twaweza kutokomeza magonjwa ya kuambukiza: WHO

Twaweza kutokomeza magonjwa ya kuambukiza: WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema magonjwa ya kuambukiza kama vile homa kali ya Ebola yanaweza kuepukika ikiwa hatua muhimu ikiwamo ushirikiano wa wadau wote katika makabiliano dhidi ya gonjwa hilo.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa, Mkurugezi wa magonjwa ya kuambukiza wa WHO ukanda wa Afrika Dkt. Magda Robalo amesema mlipuko wa Ebola waweza kutumika kama kielelezo cha namna ya kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza katika nchi zinazoendelea.

Amesema jambo muhimu la kutekeleza ili kuzuia Ebola katika nchi zinazoendelea mathalani barani Afrika ni.

( Sauti Dk Magda)

‘‘Kuendelea kufanya kazi na jamii, ili waelewe vyema namna gani wanatambua huduma za afya wanazopewa, wanataka nini katika huduma hizo na kuwafanya  washiriki kikamilifu’’

Dkt. Robalo amesema wadau wa afya wanapaswa kuondokana na fikra kwamba wanafahamu kile jamii inachokihitaji.