Umoja wa Mataifa wapongeza hatua ya Bunge Somalia

29 Disemba 2016

Umoja wa Mataifa umekaribisha hatua ya uzinduzi wa bunge jipya nchini Somalia. John Kibego na ripoti kamili.

(Taarifa ya Kibego)

Pongezi zimeelekezwa kwa wananchi wa Somalia kwa hatua hiyo adhimu ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ni hatua ya kihistoria, katika juhudi zao za kusaka haki ya kupiga kura kwa wote mwaka 2020.

Hata hivyo Ban amelitaka bunge hilo jipya kujitahidi kukamilisha mchakato wa uchaguzi haraka iwezekanavyo kwa kufanikisha uchaguzi wa Spika wa mabunge yote na hatimaye Rais wa Somalia.

Bwana Ban amepongeza ujumbe wa Umoja w aAfrika nchini Somalia (AMISOM), kwa kuweka mazingira yaliowezesha kufanyika kwa chaguzi.

Akizungumzia mwelekeo wa baadaye, Naibu ya mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini Somalia Peter de clerq amesema..

(Sauti ya deClerq)

“Tumekuwa na ushirikiano wa karibu na serikali na bunge la Somalia kwenye suala la ujenzi wa nchi na tungependa kuuendeleza sambamba na suala la uwazi na uwajibikaji. Tunatarajia kuwa tutamaliza changamoto za uchaguzi zilizojitokeza na uendeleza ushirikiano mzuri tuliokuwa nao tangu mwaka wa 2012."

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter