Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuapishwa kwa wabunge wapya ni hatua kubwa katika historia,Somalia

Kuapishwa kwa wabunge wapya ni hatua kubwa katika historia,Somalia

Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM umesema kwamba kuapishwa kwa wabunge wapya nchini humo ni hatua chanya katika historia ya nchi hiyo.

Katika taarifa yake UNSOM imesema kwamba takriban wabunge 283 wameapishwa Jumanne.

Taarifa zinasema kwamba wajumbe 41 watakuwa maseneta katika bunge la juu huku wengine 242 watakuwa wajumbe katika cbunge la wananchi.

Maspika wa bunge tayari wamechaguliwa na bunge zote.

Hatua hii inakuja baada ya wiki kadhaa za kupiga kura huku ripoti za ukiukwaji na uvunjaji sheria ikiwemo udanganyifu na ufisadi zikiripotiwa.

Jumanne jamii ya kimataifa walitoa taarifa wakielezea wasiwasi wao juu ya mchakato wa uchaguzi ambao ni wa kawanza katika miongo miwili.

Wabunge wanatarajiwa kupiga kura ya siri ya kumchagua rais.