Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani yapongezwa kwa sheria inayoheshimu uhuru wa imani

Marekani yapongezwa kwa sheria inayoheshimu uhuru wa imani

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa dini au imani, Ahmed Shaheed, amekaribisha marekebisho ya sheria ya kimataifa ya uhuru wa dini iliyotekelezwa ijumaa nchini Marekani na Rais Barack Obama, inayotambua haki za wasioamini Mungu.

Taarifa ya Bwana Shaheed imemnukuu akisema hayo ni mafanikio muhimu kwakuwa waamini Mungu na wasioamanini wanapaswa kulindwa wote hasa kwa kuzingatia kuwa wengi wa wasioamini wanayanyapaliwa duniani.

Amesema katika baadhi ya nchi, kupigia chepuo kundi hilo huchukuliwa kama kitendo cha ugaidi huku kwa nchi nyingine kujieleza kwa asiyeamaini Mungu huhukumiwakama ni uasi au kufuru na kupewa adhabu ikiwamo hukumu ya kifo au kushambuliwa na vikundi vinavyojichukulia sheria mkononi.

Mtaalamu huyo maalum wa UM ameongeza kuwa haki za kimataif a za binadamu zimekuwa hazieleweki katika muktadha wa uhuru wa dini akisema kuwa sio tu kuhusu dini au imani bali pia haki hizo zinazingatia uhuru wa mawazo na dhamiri kama ilivyoelezwa na mkataba wa kimataiafa wa haki za binadamu.