Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

2016 ulikuwa janga kwa Syria, 2017 nuru yaangazia- Pinheiro

2016 ulikuwa janga kwa Syria, 2017 nuru yaangazia- Pinheiro

Mwenyekiti wa Tume huru ya uchunguzi kuhusu Syria, Paulo Sergio Pinheiro amesema mwaka 2016 ulikuwa mwaka mbaya zaidi kwa nchi hiyo ambayo mzozo wake unakamilisha mwaka wa sita tangu kuanza. Grace Kaneyia na ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Pinheiro ameieleza Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa hali hiyo inatokana na ukweli kwamba raia wamekumbwa na mashambulizi ya kijeshi mfululizo akisema kwamba..

(Sauti ya Pinheiro)

“Kulikuwa na nyakati za nuru hasa kutokana kazi inayofanywa na mwenzangu Staffan de Mistura ya kujenga fursa ya mashauriano baina ya pande kinzani, miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka ilikuwa na matumaini lakini miezi iliyosalia imekuwa ya kukata tamaa.”

Bwana Pinheiro hata hivyo anaona kuna matumaini mwaka ujao wa 2017 akisema..

(Sauti ya Pinheiro)

Kuchaguliwa kwa Antonio Guterres kama Katibu Mkuu, kama alivyosema kwenye moja ya mahojiano kuwa Syria itakuwa ni kipaumbele chake, tunakaribisha sana hatua hii na uzoefu wake kwenye suala hilo tunaweza kuona mikakati mipya ya kuleta fursa mpya za mazungumzo.”