Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa dola zaidi ya milioni tatu na nusu kukarabati shule Haiti baada ya kimbunga Matthew

Msaada wa dola zaidi ya milioni tatu na nusu kukarabati shule Haiti baada ya kimbunga Matthew

Umoja wa Mataifa umeipatia Haiti msaada wa dola zaidi ya Milioni tatu na nusu kwa ajili ya ukarabati wa shule ambazo ziliharibiwa na kimbunga Matthew.

Fedha hizo pia zinalenga kusaidia watu wapatao Elfu 30 ambao wanarejea kwenye maeneo yao kutoka kwenye shule hizo ambako walikimbilia kusaka hifadhi na huduma za msingi baada ya janga hilo.

Fedha hizo ni kupigia mfuko wa majanga wa Umoja wa Mataifa, CERF ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF litaongoza utekelezaji wa mradi wa elimu kwenye maeneo ya Les Cayes, Port Salut na Jeremie.