Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Poland mwenyeji wa mkutano wa utalii endelevu: UNTWO

Poland mwenyeji wa mkutano wa utalii endelevu: UNTWO

Sambamba na maadhimisho ya mwaka wa utalii endelevu kwa maendeleo yanayotarajiwa  kuadhimishwa mwaka 2017, mkutano wa tatu kuhusu maadili na utamaduni utafanyika nchini Poland mnamo april 27 hadi 28 mwakani.

Hii ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na utalii duniani UNWTO, linaloratibu maandalizi kwa kushirikiana na Tume ya Ulaya EU, na serikali ya Poland ambapo mkutano huo utajikita katika jukumu la pamoja la wadau katika kupigia chepuo sekta ya utalii endelevu.

Mkutano huo pia utaangazia malengo ya maendeleo endelevu SDGs  hasa masuala ya utawala na uwajibikaji wa kijamii (CSR), uwajibikaji wa  matumizi, fursa kwa wote kama ufanisi usimamizi wa maliasili na utamaduni.

Kwa mujibu wa UNTWO, sekta ya utalii inahitaji kujenga ushirikiano mzuri na kupitisha sera madhubuti za kitaifa na mikakati endelevu ya biashara katika maeneo yote ya maendeleo.