Raia bado wana hali tete Iraq: OCHA

27 Disemba 2016

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA imesema  zaidi ya watu 100,000 waliofurushwa makwao, wengine 10,000 ambao wamerejea makwao na mamia kwa maelfu bado wanahitaji masaada nchini Iraq.

Kwa mujibu wa tathimini ya OCHA kuhusu athari za kivita nchini humo, wakati mamilioni ya raia wakiwa hawajafikiwa ili kupatiwa msaada mjini Mosul, mahitaji makubwa humo ni ukosefu wa chakula na maji.  

Athari za kisaokolojia, majeruha, yanasalia madhila kwa raia hussuani Mashariki mwa mji wa Mosul, ambapo zaidi ya 900 wamejeruhiwa kutokana na risais, mabomu ya kutegwa ardhini na moto.

wasio na makazi 114,042, karibu 10,000 wamerejea makwao lakini mamia ya maelfu ya wakazi wengine kwenye mazingira magumu bado wanahitaji msaada.

Inakadiriwa kuwa watu wapatao milioni moja watu hawajapata  misaada ya kibinadamu katika mji Mosul  na zaidi taarifa hiyo imesema kuna upungufu wa chakula na maji.

Hili ni ongezeko kubwa kwa idadi ya 661 kulinganisha na juma lililopita.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter