Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO wakabiliana na ukeketaji Tanzania

UNESCO wakabiliana na ukeketaji Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO nchini Tanzania, kwa kushirikiana na wadau wengine wanasaidia jamii nchini humo kukabiliana na mbinu mpya ya ukeketaji inayowahusisha watoto mkoani Dodoma.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii, Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya UNESCO , Dk. Moshi Kimizi amesema licha ya juhudi zilizofanywa dhidi ya vitendo hivyo ambavyo vinakiuka haki za binadamu, bado vinaendelea kuathiri jamii.

(SAUTI KIMIZI)

Ametaja hatua ambazo zinachukuliwa na UNESCO hususani wilayani Kondoa ambako ukeketaji umeshamiri.

(SAUTI KIMIZI)