Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wapitisha azimio kulaani Israel kujenga makazi

UM wapitisha azimio kulaani Israel kujenga makazi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepitisha azimio kuhusu makazi ya Israeli kwenye eneo linalokalia la wapalestina likieleza kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa.

Azimio hilo limepitishwa na nchi 14 wanachama wa baraza hilo wakati Marekani haikupiga kura.

Azimio hilo pamoja na mambo mengine linataka Israel mara moja kusitisha shughuli zozote za ujenzi, kitendo ambacho wamesema kwa kusitisha kutaonyesha nia njema katika utekelezaji wa hoja ya mataifa mawili kuwepo pamoja; Palestina na Israeli.

Azimio pia linataka kuchagizwa kwa harakati za kitaifa, kimataifa na kikanda ili kufanikisha amani ya kudumu kati ya mataifa hayo mawili.