Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunahofia mashtaka dhidi ya mpigania haki za binadamu Bahrain: OHCHR

Tunahofia mashtaka dhidi ya mpigania haki za binadamu Bahrain: OHCHR

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu OHCHR imesema ina wasiwasi kuhusu mashtaka yanayoendelea juu ya Nabeel Rajab mmoja wa wanzilishi wa kituo cha haki za binadamu nchini Bahrain ambaye amekuwa kizuizini tangu Juni 13 mwaka huu kwa ajili ya kutekeleza haki yake ya uhuru wa kujieleza.

Rajab anakabiliwa na mashtaka mengi yanayohusiana na maoni kwenye mtandao wa twita aliyoandika kuhusu mateso gerezani na kukosoa mashambulizi ya anga ya Saudi Arabia nchini Yemen,makosa ambayo hukumu yake ni kifungo cha miaka 10 na tatu gerezani

Taarifa ya OHCHR inasema kuwa mnamo Septemba tano aliongezewa shtaka jingine la kutangaza taarifa za uwongo kwa makususi na tetesi ambazo zilidhalilisha taifa lake.

Mwendesha mashataka mkuu aliwaslisha mashataka hayo kwa kuzingatia makala yake katika gazeti la New York Times.

Ofisi hiyo ya haki za bianadamu ya Umoja wa Mataifa imeitaka Bahrain kumwachia Bwana Rajab hima, kwakuwa kuikosoa seikali sio kigezo cha kuwekwa kizuizini na kushitakiwa.