Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa na usaidizi nchini Burundi kwa mwaka huu wa 2016

Umoja wa Mataifa na usaidizi nchini Burundi kwa mwaka huu wa 2016

Katika mfululizo wa makala za kuangazia kazi za Umoja wa Mataifa katika ukanda wa nchi za maziwa makuu, tumejikita Burundi nchi ambayo mwaka jana ilikumbwa na sintofahamu ya kisiasa kabla na baada ya uchaguzi mkuu.

Umoja wa Mataifa kupitia Baraza la Usalama, na wawakilishi wake walifanya kazi ngumu ya kusaka suluhu ya kisiasa baada ya Rais wa nchi hiyo Piere Nkurunzinza kugombea mhula wa tatu wa Urais licha ya utata wa katiba, hatua iliyozua tafrani katika taifa hilo la kwani upinzani ulisusuia uchaguzi ukipinga hatua hiyo na hivyo kuzua machafuko.

Burundi pia imeshuhudia wimbi la wakimbizi waliosaka hifadhi nje ya nchi baada ya machafuko na huku shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR, likikadiria kuwa taifa hilo pia linahifadhi wakimbizi zaidi ya 50,000 wa nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC

Kutoka Bujumbura  mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga anasimulia hayo na mengine mengi ambayo UM umejihusisha nayo mwaka huu wa 2016 unapomalizika.