Raia 40 wauawa katika maandamano DRC wiki hii

23 Disemba 2016

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Zeid Ra’ad Al Hussein amesema ripoti ya mauaji ya takriban raia 40 wiki hii huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC kwa sababu ya maandamano dhidi ya Rais Joseph Kabila ni jambo la kushtua na linadhihirisha hali ya wasiwasi nchini humo. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Ripoti ya ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu nchini DRC imeandikisha mauaji ya raia 40 huko Kinshasa, Lubumbashi, Boma na Matadi pamoja na majeruhi 107 huku wengine 460 wakitiwa korokoroni wakati wa maandamano .

Elisabeth Throssel ni Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu, Geneva, Uswisi...

(Sauti ya Elisabeth)

"Kushindwa kwa mamlaka ya DRC na vikosi vya usalama kutekeleza wajibu wao wa kimataifa wa kuhakikisha watu wana haki ya uhuru wa kujieleza, ya kujiunga na vyama na hata kukusanyika ni lazima vikemewe”.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter