Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sasa ni fursa ya kuanza mazunguzo ya Syria- UM

Sasa ni fursa ya kuanza mazunguzo ya Syria- UM

Muda ukisonga kasi huko Aleppo nchini Syria kuondoa maelfu ya watu walionada kwenye maeneo ya mapigano yaliyozingirwa.

Hatua hiyo inaendelea baada ya Baraza la Usalama kupitisha azimio la kupeleka waangalizi kusimamia uhamishaji wa raia hao.

Kufuatia hatua hiyo mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Staffan de Mistura amesema sasa ni fursa ya kuchagiza mazungumzo mapya ili kumaliza mzozo unaoendelea nchini humo.

(Sauti ya de Mistura)

“Sasa ni wakati wa kuzindua tena majadiliano ya kisiasa, ili kuhakikisha kuna kasi kulingana na umoja mpya wa baraza la usalama. Tunatangaza kwamba Februari nane hapa Geneva, tuaanza majadiliano ya upatanishi  wa kisiasa kwa ajili ya Syria.