Maï-Maï Nyatura waua watu 20 huko Kivu Kaskazini

Maï-Maï Nyatura waua watu 20 huko Kivu Kaskazini

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC watu 20 wameripotiwa kuuawa katika shambulio linalodaiwa kutekelezwa na wapiganaji wa Maï-Maï Nyatura huko Rutshuru, jimbo la Kivu Kaskazini. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Watu walioshuhudia shambulio hilo la Jumatano wamesema wapiganaji hao wa kihutu walivamia mji wa Bwalanda wakiwa na silaha ambapo pamoja na kuua watu, walichoma moto nyumba za watu wa jamii ya Nande.

Radio Okapi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko DRC, MONUSCO imesema jitihada za jeshi kukabiliana na Mai Mai Nyatura ziligonga mwamba kutokana na uwezo waliokuwa nao wapiganaji hao ambao hatimaye walirejea makazi yao ya Nyanzale.

Shambulio hili limekuja baada ya jeshi la serikali kubaini maiti watatu ya raia karibu na eneo hilo hapo jana.