Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa kusaidia wakimbizi wa kisomali Kenya wapata dola milioni tatu

Mradi wa kusaidia wakimbizi wa kisomali Kenya wapata dola milioni tatu

Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa ujenzi wa amani umeidhinisha dola milioni tatu kwa ajili ya mradi wa majaribio wa kuwapatia stadi za ufundi na wakimbizi wa Somalia wanaorudi makwao kwa hiari kutoka Kenya.

Fedha hizi zitatumika kuwandaa kuchangia mchakato wa ujenzi wa amani nchini mwao na pia kutangamana na jamii zao.

Taarifa ya mfuko huko imesema mradi huo ni wa kipekee na unawalenga waliovuka mpaka, na pia wale walio kwenye kambi ya Dadaab, nchini Kenya na hata waliorudi Baidoa nchini Somalia kupitia makubaliano kati ya serikali ya Kenya na Somalia na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Hatua hii ya kukuza mshikamano na azimio la amani juu ya mgogoro wa Somalia na inapatia vipaumbele juhudi za serikali za kuleta utulivu na amani ikiwa ni pamoja na uwekezaji katika ajira.

Fedha hizo zitapatiwa UNHCR nchini Kenya na mashirika mengine kama vile UNICEF, FAO, WFP, IOM na ILO nchini Somalia.

Mfuko huo wa ujenzi unadhamini miradi mingine nchini Somalia kwa lengo la kuimarisha mamlaka ya kitaifa katika maeneo yaliyokombolewa kutoka kwa wapinzani wa serikali.