Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watu palestina kuongezeka maradufu ifikapo 2050-UNFPA

Idadi ya watu palestina kuongezeka maradufu ifikapo 2050-UNFPA

Shirika la Umoja wa mataifa la idadi ya watu UNFPA limetoa ripoti inayoonyesha kwamba idadi ya watu katika maeneo yaliyokaliwa ya Palestina itaongezeka kwa milioni 2.2 kufikia mwaka 2030 na maradufu kufikia 2050 kutoka 4.7 milioni hadi 9.5.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo iitwayo Palestina 2030: ‘mabadiliko ya mwenendo wa idadi ya watu fursa za ukuaji’ mwakilishi wa UNFPA huko Palestina, Anders Thomsen amesema idadi ya watu itongezeka katika ukanda wa Gaza na maeneo yanayokaliwa ya Palestina na kufikia takriban watu milioni 5 kufikia mwaka 2030.

Huku dunia ikitarajia kufikia malengo ya mwaka 2030 ambayo inasisitiza kwamba hakuna mtu anayepaswa kuachwa nyuma Bwana Thomsen amesema…

(Sauti ya Anders)

“Ni vigumu kufikiria jinsi ya kubuni fursa za kiuchumi na kazi ili kuenda sambamba na huduma za kijamii, na idadi ya watu inayoongezeka bila kuwepo mazungumzo na jamii ya kimataifa ikiwemo Israeli kuhusu mbinu za kuondoa vikwazo na kuwezesha usafiri huru wa bidhaa na watu.”

Ukosefu wa ajira katika ukanda wa Gaza ni asilimia 4.3 na fursa za kazi milioni moja zinahitaji kubuniwa ili kuweza kukidhi mahitaji yaliyopo sasa.