Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa mafuta waafikiwa baini Sudan na Sudan Kusini

Mkataba wa mafuta waafikiwa baini Sudan na Sudan Kusini

Serikali za Sudan Kusini na Sudan wamefikia makubaliano ya kuongeza mkataba wa ushirikiano katika sekta ya mafuta ya petroli kwa muda miaka mitatu, baada ya mazungumzo ya siku mbili baina ya nchi hizo mbili jijini Khartoum, Sudan. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Radio Miraya ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini, UNMISS imeripoti kuwa Waziri wa Petroli wa Sudan Kusini, Ezekiel Lol Gathkuot amesema makubaliano hayo ni pamoja na marekebisho ya Mkataba wa Mpito wa Fedha, ambayo mwaka 2012 serikali yake yenye kuchukua asilimia 75 ya mapato ya mafuta ilikubali kuilipa serikali ya Sudan dola zaidi ya bilioni Tatu katika miaka mitatu, fedha ambazo serikali yake bado haijaweza kulipa.

Amesema makubaliano mengine ni Sudan kufungua tena uzalishaji katika eneo la pamoja la mafuta la UNITY, na vile vile kusaidia nchi yake kujenga uwezo wa wahandisi.

Kuhusu suala la ulinzi wa usalama kwa wafanyakazi wa pande hizo mbili, amesema..

(Sauti ya Ezekie)

"Tumekubaliana kuwa kutakuwa na uratibu wa pamoja baina ya nchi hizo mbili kuhakikisha wafanyakazi kutoka pande zote mbili watalindwa".