Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njaa yaathiri uchumi wa Madagascar

Njaa yaathiri uchumi wa Madagascar

Utafiti kuhusu namna njaa inavyoligharimu bara la Afrika COHA, unaonyesha kuwa ukosefu wa chakula huathiri kwa kiwango kikubwa uchumi wa taifa la Madagascar ambapo hupoteza dola bilioni moja na nusu kwa mwaka. Joseph Msami na maelezo kamili.

(TAARIFA YA MSAMI)

Matokeo ya utafiti huo ulioendeshwa kwa ushirikiano kati ya shirika la mpango wa chakula duniani WFP, kamisheni ya Muungano wa Afrika na mpango mpya kwa maendeleo ya Afrika NEPAD ,unaonyesha kuwa kiwango hicho kinachopotea kwa mwaka ni sawa na asilimia 14 nukta tano ya mapato ya ndani ya Madagascar.

Utafiti umeangazia zaidi athari za kijamii,kiuchumi zinazosababishwa na utapiamlo katika nchi hiyo ambayo iko katika orodha ya nchi zenye uchumi tegemezi duniani LDCs.

Kufuatia matokeo ya COHA, yaliyowasilishwa rasmi leo kwa Waziri Mkuu wa Madagascar na kamisheni ya Muungano wa Afrika, kiongozi huyo ametaka usaidizi zaidi katika kuwekeza ili kukabiliana na utapiamlo sugu.