Magaidi husafirisha watu na kutekeleza ukatili wa kingono, tuchukue hatua-Ban

20 Disemba 2016

Baraza la usalama leo limekuwa na mjadala wa ngazi ya mawaziri kuhusu usafirishaji haramu wa watu katika maeneo yenye mizozo, mada inayohusiana na kulinda amani ya kimataifa na usalama.

Akizungumza katika majadala huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema licha ya kwamba usafirishaji haramu unavuka mipaka, waathirika zaidi ni wale walioko katika mizozo hususani wanawake, watoto, wakimbizi wa ndani na wakimbizi.

Ban amesema magaidi hutumia mwanya huo kuchomoza na kutesa watu huku akitolea mfano.

(Sauti Ban)

‘‘ISIL ,Boko Haram na wengineo wanatumia usafirishaji haramu na ukatili wa kingono kama silaha na chanzo muhimu cha mapato.’’

Ametoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka ikiwamo nchi kupitisha sheria madhubuti na mikakati ya kitaifa pamoja na kuanzisha ofsi maalum ya waendesha kuhusu usafirishaji haramu na ya ukatili wa kingono.

Miongoni mwa wadau waliohudhuria na kuchangia katika mjadala huo ni mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kigono katika maeneo yenye mizozo Zeinab Bangura na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu madawa na uhalifu Yury Fedetov.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter