Balozi wa Urusi nchini Uturuki auawa, UM walaani

19 Disemba 2016

Balozi wa Urusi nchini Uturuki Andrey Karlov ameuawa kwenye mji mkuu Ankara.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa mtu mmoja aliyekuwa na silaha alimpiga risasi balozi Karlov jumatatu jioni kwa saa za Uturuki wakati wa maonyesho , ambapo hata hivyo mtu huyo yaripotiwa aliuawa na maafisa wa polisi.

Ban kupitia taarifa ya msemaji wake amelaani kitendo hicho akituma salamu za rambirambi kwa familia ya balozi Karlov na serikali ya Urusi.

Amesema anasikitishwa na kitendo hicho cha kigaidi na kusisitiza kuwa hakuna jambo lolote linaloweza kuhalalisha mauaji ya raia na wanadiplomasia.

Katibu Mkuu anafuatilia kwa karibu hali inavyoendelea huku akiwatakia ahueni ya haraka wale wote waliojeruhiwa kwenye shambulio hilo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter