Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO na kongamano la sayansi endelevu.

UNESCO na kongamano la sayansi endelevu.

Shirika la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO linafanya kongamano kuhusu matumizi ya sayansi endelevu mjini Kuala Lumpur, nchini Malaysia, lililoanza leo Desemba 19 hadi Desemba 21.

Lengo kuu la mradi huo ni kwa ajili ya kukuza mjadala na kusambaza ujumbe wa sera thabiti  ambayo itasaidia nchi wanachama wa UNESCO kuanzisha mbinu za sayansi katika kukabiliana na changamoto kote duniani. Na kuendeleza seti ya miongozo kutoka kwa ufafanuzi katika mwisho wa 2017.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNESCO, kongamano hili itaruhusu kutambua mahitaji na upungufu hasa kwa kila kanda na kuipatia kipaumbele ili kuchukua hatua kwa ajili miongozo ya kisera iliyopangwa juu ya matumizi ya sayansi endelevu na kutoa fursa kwa masuala yanayoshabihiana na mada hiyo  yakiwa maalum kwa kila mkoa.

Mnamo Oktoba 2015, idara ya UNESCO inayohusika na asili na sayansi ya jamii na sekta ya binadamu pamoja na Wizara ya Elimu, Utamaduni, Michezo, Sayansi na Teknolojia ya Japani ilianzisha mradi wa upanuzi wa miundo mbinu ya sayansi endelevu ikizingatia ajenda ya 2030 ajenda ya maendeleo endelevu.