UNICEF yasaida kuunganisha watoto wa Aleppo na familia zao

19 Disemba 2016

Watoto 47 waliokuwa wamenasa kwenye kituo cha watoto yatima huko Mashariki mwa Aleppo wameokolewa na wako salama ingawa wengine wana majeraha.

Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Geert Cappelaere amesema hayo leo akieleza kuwa wengine wanakabiliwa na ukosefu wa maji mwilini.

Amesema wanachofanya sasa kwa kushirikiana na wadau ni kusaidia kuwaunganisha watoto hao na wengine waliookolewa hivi karibuni kuungana na familia zao.

Halikadhalika kuwapatia huduma za haraka za matibabu na nguo za baridi zinazohitajika ikiwa bado kuna habari kuwa wengi wao katika mazingira magumu.

UNICEF imekumbusha pande zote ya majukumu yao chini ya sheria za kimataifa ya kuwalinda watoto, popote pale walipo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter