Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu lapitisha azimio la kusaidia Haiti kupambana na Kipindupindu

Baraza Kuu lapitisha azimio la kusaidia Haiti kupambana na Kipindupindu

Leo Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa makubaliano azimio nambari A/71/L42 la kuunga mkono mbinu mpya ya umoja huo kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu nchini Haiti.

Azimio hilo linafuatia mpango wa Katibu Mkuu Ban Ki-moon mapema mwezi huu lililoweka awamu mbili za usaidizi kwa wananchi wa Haiti.

Mpango huo mpya una lengo la kuongeza msaada kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa huduma na matibabu ya ugonjwa wa Kipindu pindu na hatimaye kuondoa maambukizi nchini ikiwa ni pamoja na mupangilio wa muda mfupi na mrefu juu ya mifumo ya maji, usafi wa mazingira na afya.

Pia inataka kutoa msaada wa vifaa na msaada kwa raia wa Haiti zaidi moja kwa moja kwa walioathirika na hasa walioathirika na ugonjwa na familia zao kupitia kwa serikali na mashirika yasiyokuwa ya serikali.

Azimio hilo pamoja na mambo mengine linatambua wajibu wa maadili ya Umoja wa Mataifa kwa waathirika wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Haiti na liliwasilishwa na mwakilishi wa kudumu wa Uruguay kwenye Umoja wa Mataifa kwa niaba ya nchi yake na marafiki wa Haiti.

Tangu mwaka 2010, mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu umewaathiri takriban watu 800,000 na kusababisha vifo vya zaidi watu 9,000 kufikia sasa.

Kimbunga Matthew kilichopiga nchi hiyo mnamo Oktoba 4 mwaka huu, uliongezea idadi ya watu walioathirika na ugonjwa huo ikiwa na pamoja na gharama inayokadiriwa kufika dola milioni 400 kwa muda wa zaidi ya miaka miwili ijayo.