Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi za Umoja wa Mataifa nchini Uganda kwa mwaka huu wa 2016

Kazi za Umoja wa Mataifa nchini Uganda kwa mwaka huu wa 2016

Umoja wa Mataifa  umejikita nchini Uganda katika shughuli kadhaa za usaidizi wa masuala ya kibinadamu pamoja na miradi ya maendeleo, ambapo mashirika kadhaa kama vile shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR, mpango wa chakula WFP, la kuhudumia watoto UNICEF nakadhalika yamejikita humo.

Miongoni mwa mambo makuu yanayofanywa na umoja huo ni usaidizi kwa malefu ya wakimbizi kutoka nchi jirani ambazo zimekumbwa na machafuko ikiwamo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Burundi na Sudan Kusini.

Mzigo mkubwa ambao taifa hilo linabeba ni wakimbizi wa Sudan Kusini ,wakati huu mzozo huo ukiingia mwaka wanne. Kwa mujibu wa UNHCR, Uganda inahifadhi wakimbizi karibu milioni moja na hivyo kuwa taifa la tatu barani Afrika kwa kuhifadhi idadi kubwa ya wakimbizi.

Tunaungana na John Kibego kutoka nchini humo kwa makala inayofafanua yaliyojiri katika  za shughuli za mashirika ya Umoja wa Matifa hasa pilikapilika ya kuhudumia wakimbizi wa Sudan Kusini kwa mwaka huu wa 2016 unaoekea ukingoni.