Kuwapatia fedha wakimbizi kwabadili maisha yao na wenyeji- UNHCR

16 Disemba 2016

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema kumekuwepo na mabadiliko makubwa kwenye mwenenedo wa kushughulikia janga la wakimbizi.

Mabadiliko hayo yametokana na vile ambavyo wakimbizi wanapatiwa moja kwa moja fedha ambazo kwazo wanatumia kukimu maisha yao.

Msemaji wa UNHCR, Geneva, Uswisi Adrian Edwards ametolea mfano kuwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu zaidi ya dola milioni 430 zitakuwa zimekwenda moja kwa moja kwa wakimbizi kwenye nchi 60 duniani.

(Sauti ya Adrian)

“Watu wanaweza kununua chakula chao wenyewe, mafuta, nguo, dawa na wanaweza kulipa pango, wanaweza kufanya lolote wanalotaka, kwa kuzingatia vipaumbele vyao. Mbinu hii pia imenufaisha uchumi kwa nchi walizomo na inajenga uhusiano bora na wenyeji.”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud