Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misri acheni kukandamiza watetezi wa haki wanawake- Wataalam  

Misri acheni kukandamiza watetezi wa haki wanawake- Wataalam  

Kundi la wataalam maalum wa Umoja wa Mataifa hii leo wamelaani vikali Misri kwa kitendo cha kutumia msako wao dhidi ya mashirika ya kiraia kukandamiza wanawake watetezi wa haki za binadamu na makundi yanayotetea haki za wanawake .

Hii ni kwa mujibu ya taarifa yao kutoka Geneva, Uswisi ambapo wataalamu hao wamesema hatua ya serikali inawazuia wanawake watetezi wa haki za binadamu kufanya shughuli zao halali ambapo maelfu ya wanawake wanahitaji usaidizi na usalama

Wameongeza kuwa kitanzi kinaimarishwa dhidi ya harakati za haki za wanawake , wakiseka kitendo hicho kitakuwa na madhara kwenye haki za binadamu.

Wametaja baadhi ya watetezi hao akiwemo Mozn Hassan na mwanasheria mwingine Azza Soliman, mtetezi maarufu wa haki za binadamu aliyeanzisha kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake Misri na yuko kizuizini tangu tarehe saba mwezi huu.

Wametoa wito kwa serikali ya Misri ifute mikakati yote kandamizi zote ikiwa ni pamoja na zuio la safari kwa watetezi hao na sheria za makosa ya jinai zinazoharamisha shughuli halali wakisema sheria hizo zinakinzana na wajibu wa Misri kwenye sheria za kimataifa za haki za binadamu.