Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatujakata tamaa na uokozi wa raia Aleppo: UM

Hatujakata tamaa na uokozi wa raia Aleppo: UM

Baada ya mkwamo wa uokozi kwa wakazi wa Aleppo hususani Mashariki mwa mji huo waliozingirwa na vikosi vyenye silaha , Umoja wa Mataifa umesisitiza kutokata tamaa, na kusema pande kinzani nchini Syria zimekubaliana tena kutekeelza ahadi hiyo.

Akizungumza mjini Geneva, Uswisi, mratibu wa kikao cha kikosi kazi cha kimataifa kuhusu Syria, Jan Egeland amesema asubuhi ya leo Umoja wa Mataifa uliakiwa katika makubaliano yaliyofikiwa miongoni mwa pande kinzani na hivyo kufuatilia fursa za uokozi kwa raia hao ambao wengi wamejeruhiwa.

Amesema jukumu la Umoja wa Mataifa kufutia hatu hiyo ni.

( Sauti Egeland)

‘‘Tuko tayari na tuna timu kadhaa za wataaamu katika ulinzi wa masuala ya sheria na kanuni za kibinadmu. Tuko tayari kusindikiza wale wanaookolewa, sio tu Aleppo Mashariki bali pia Idlip ambako kunadhibitiwa na vikosi vya upinzani, hapo ndipo watakapofikia manusura.’’