Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kwenye ripoti huko Jamhuri ya Afrika ya kati

Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kwenye ripoti huko Jamhuri ya Afrika ya kati

 Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA mjini Bangui umetoa ripoti yake kuhusu hali ya haki za binadamu nchini humo, iliyobaini zaidi ya visa 2,000 vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu  kati ya Juni mosi, 2015 na Machi 31 2016 ikiwa ni pamoja na miezi sita ya mwisho ya serikali ya mpito.

Baadhi ya visa hivyo ni  mauaji ya kiholela, mateso ya kinyama ya kudhalilisha na ukatili wa kijinsia, wahusika wakitajwa kuwa vikundi vya kigaidi vya zamani vya Balaka, ex-Seleka, LRA na vikundi vingine.

Wakati wa kipindi cha ripoti hiyo inaonyesha kulikuwa na ongezeka la mashambulizi na kikundi cha LRA cha Uganda, kusini mwa nchi hiyo. Pia inasemekana kuwa vikosi vya ulinzi na usalama vya serikali vilihusika na mauaji holela, kukamatwa kwa watu kiholela na kuwatia kizuizini.

Ripoti imeongezea kuwa vyombo vya ulinzi wa raia vilikwamishwa na kuwepo kwa asasi za serikali hasa nje ya mji mkuu wa Bangui na hivyo kusababisha madhara dhidi ya ukiukwaji.