Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeid asikitishwa na sitisho la kukwamua raia Aleppo

Zeid asikitishwa na sitisho la kukwamua raia Aleppo

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad al Hussein leo ameelezea masikitiko yake kufuatia mkwamo wa mpango wa kuwakwamua maelefu ya raia mjini Aleppo nchni Syrai wakiwamo wagonjwa na majeruhi .

Katika taarifa yake Kamishna Zeid amesema wakati sababu za kuvunjika kwa sitisho la mapigano zikiwa zenye utata bado, mashambulizi mapya ya anga yanayotekelezwa na vikosi vya serikali na washirika wake katika meneo yeliyosheheni raia yanaelekea kuwa uhalifu wa sheria za kimataifa na kuendeleza uhalifu wa kivita.

Amekaririwa akisema kuwa uokoaji wa raia Mashariki mwa Aleppo laziam ufanyike kwa kuzingatia sheria za kimataifan na kwamba serikali ya Syria ina wajibu wa kuhakikisha kuwa watu wake wako salama na inaelekea kushindwa kuutekeleza wajibu huo.

Kamishna Zeid amesema mpango wa kuwakwamua raia ambao uliwapa matumaini ya kuiona siku nyingine na kisha kukatishwa katika kipindi cha nusu siku ni ukatili dhidi ya raia hao.