Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya usalama Afrika yatawala mazungumzo ya Ban na Sam Kutesa wa Uganda

Hali ya usalama Afrika yatawala mazungumzo ya Ban na Sam Kutesa wa Uganda

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Uganda Sam Kutesa. Wawili hao wamebadilishana mawazo kuhusu masuala ya amani, usalama na changamoto za kibinadamu zinazoikabili Uganda ikiwa ni pamoja na maendeleo ya karibuni ya Sudan Kusini, Somalia, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Burundi.

Katibu Mkuu ameishukuru Uganda kwa mchango wake nchini Somalia, kupitia askari wa kulinda amani wa Muungano wa Afrika (AMISOM), pia kwa kusaidia kuhakikisha mazingiza bora ya kufanyika uchaguzi nchini humo.

Pia amezungumzia umuhimu wa ushirika baiana ya Umoja wa Mataifa na Uganda  katika mchakato wa amani nchini Sudan Kusini na amesisitiza haja ya kukoma haraka vitendo vya uhasama na kudumisha juhudi za amani.

Ban amepongeza ukarimu wa Uganda kwa kupokea wimbi kubwa la wakimbizi na kuwahifadhi.