Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazingira kama yale ya mauaji ya kimbari Rwanda yananyemelea Sudan Kusini

Mazingira kama yale ya mauaji ya kimbari Rwanda yananyemelea Sudan Kusini

Nchini Sudan Kusini , hatari ya mauaji ya kimbari ni dhahiri kama ilivyokuwa Rwanda na jumuiya ya kimataifa ni lazima ichukue hatua haraka kuzui hilo.

Huo ni ujumbe kutoka kwa wataalamu kwenye baraza la haki z binadamu la Umoja wa Mataifa lililofanya kikao maalumu mjini Geneva Jumatano kuhusu madhila katika taifa hilo change kabisa duiniani

Vita vya silaha katika misingi ya kikabila vimelighubika taifa hilo tangu 2013 na sasa kuna hofu kwamba mazingira yako tayari kwa mauaji ya kimbari yanayolinganishwa na Rwanda ambako watu zaidi ya laki nane waliuawa katika kipindi cha chini ya miezi mitatu mwaka 1992.

Yasmin Sooka anaongoza timu ya haki za binadamu ya uchunguzi Sudan Kusini

(SAUTI YA YASMIN)

“Kila tulipowatembelea watu walituambia nchi itatumbukia katika hali ya Rwanda nyingine. Wakati dalili za awali za mauaji ya kimbari zipo hilo halimaaninishi haliwezi kuepukika. Na hakika linahitaji kuchukuliwa hatua sasa.”

Vita vilivyoshika kasi Julai mwaka huu vimewalazimisha zaidi ya watu milioni tatu kukimbia makwao na Umoja wa Mataifa umeonya kwamba takribani watu milioni 4.6 watahitaji msaada wa wa chakula mwezi ujao wa Januari.