Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzalishaji mbao wahuhudia ongezeko kutokana na soko la nyumba na nishati mbadala:

Uzalishaji mbao wahuhudia ongezeko kutokana na soko la nyumba na nishati mbadala:

Uzalishaji wa kimataifa wa mbao katika maeneo yote makubwa ya bidhaa za mbao umekuwa kwa mwaka wa sita mfululizzo mwaka 2015 huku biashara ya bidhaa za mbao ikipungua kidogo kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo Jumatano na shirika la chakula na kilimo FAO.

Ongezeko hilo limechagizwa na kuendelea kukua kwa uchumi Asia, kuibuka tena kwa soko la nyumba Amerika ya Kaskazini na kuongezeka juhudi za malengo ya nishati mbadala.

Takwimu hizo mpya za FAO zinasema mwaka 2015 ukuaji wa kiwango cha uzalishaji wa bidhaa za mbao ulikuwa ni kati ya asilimia moja hadi nane.

Wakati huohuo thamani ya biashara ya kimataifa ya mbao na bidhaa za karatasi imesinyaa kidogo kutoka dola bilioni 267 mwaka 2014 na kufikia dola bilioni 236 mwaka 2015 kutokana na bei ndogo ya bidhaa za mbao. Uzalishaji wa bidhaa za misitu umekuwa na tija ukanda wa Asia-Pacific na Amerika Kaskazini kutokana na kukua tena kwa soko la nyumba.