Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji katika sayansi na teknolojia kwa kilimo ni muhimu ili kuondoa njaa: FAO

Uwekezaji katika sayansi na teknolojia kwa kilimo ni muhimu ili kuondoa njaa: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani limesema leo kuwa ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu na kushinda njaa na umaskini ifikapo mwaka 2030, serikali na sekta binafsi zina haja ya kuongeza uwekezaji wa sayansi na teknolojia kwa kilimo, uwezo na utafiti.

Mkurugenzi msaidizi mkuu na mwakilishi wa mkoa kwa Asia na Pasifiki Kundhavi Kadiresan aliyasema hayo kwenye mkutano wa tisa wa kimataifa wa viongozi na wa sayansi na teknolojia kwa kilimo iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chuo cha Kichina cha Sayansi na Kilimo na FAO katika mkoa wa Hainan, China.

Katika ripoti yake tofauti iliyotolewa wiki iliyopita na FAO ofisi ya kanda ya Asia na Pasifiki, shirika hilo limeonya kuwa uwekezaji katika utafiti wa kilimo usipoongezeka, hasa katika Asia iliyo na asilimia 60 ya watu wanaokumbwa na njaa duniani, juhudi za kimataifa ili kutimiza kufikia lengo la kufikia sifuri ifikapo mwaka 2030 itapunguka.

Kadiresan amesema ikiwa kuna watu takriban milioni 800 walio na njaa na utapiamlo ulimwenguni, uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia kwa kilimo unahitajika zaidi kuliko hapo awali liki upunguza njaa na umaskini, kuleta mafanikio na kuongeza tija katika kilimo

FAO ina makadirio kuwa dunia itahitaji wastani wa asilimia 60 ya uzalishaji wa chakula, kulisha dunia ambayo ifikapo mwaka 2050 idadi ya watu inatarajiwa kuwa bilioni tisa.