Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto yazinduliwa Tanzania

Kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto yazinduliwa Tanzania

Asilimia 30 ya wasichana kati ya miaka 13 hadi 24 nchini Tanzania wamefanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kutimiza miaka 18, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Takwimu hizi ni miongoni mwa sababu za kampeni maalum ya kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana iliyozinduliwa wilayani Pangani mkoani Tanga, kaskazini mwa Tanzania. Ungana na Martha James wa redio washirika Pangani Fm ya mkoani humo anayekusimulia mkasa wa mtoto aliyenajisiwa.