Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi ya lugha yazusha tafran Cameroon

Matumizi ya lugha yazusha tafran Cameroon

Watu wanne wameuwawa nchini Cameroon baada ya purukushani na polisi wakati wa maandamano katika mji wenye kutumia lugha ya kiingereza wa Bamenda yaliyotokea Disemba 08.

Hayo ni kwa mujibu wa Ofisi ya haki za binadamu ambayo imetoa wito hii leo kwa serikali ya nchi hiyo kufanya uchunguzi huru kwa ufanisi na kwa haraka kuhusu mauaji hayo.

Ofisi hiyo inasema maandamano hayo ni moja ya misururu ya maandamano mjini Bamenda, baada ya walimu, wanafunzi na mawakili wa mji huo kukataa matumizi ya lugha ya kifaransa mashuleni na mahakamani.

Elisabeth Throssell ni msemaji wa OHCHR, Geneva...

(Sauti ya Elisabeth)

"Tunatoa wito kwa mamlaka ya Cameroon kuhakikisha kwamba vikosi vya usalama vinajizuia na matumizi ya kupindukia ya silaha wakati wa maandamano, na kwamba haki ya huru ya kujieleza kwa amani inaheshimiwa. Pia tunatoa wito kwa waandamanaji kuandamana kwa amani na sio kwa vurugu."