Kongamano la uhamiaji na maendeleo lafunga pazia Bangladesh

13 Disemba 2016

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM Bwana William Lacy Swing amekaribisha matokeo ya kongamano la 9 la kimataifa kuhusu uhamiaji na maendeleo.

Kongamano hilo la siku tatu lililofunga pazia jumatatu mjini Dhaka Bangladesh lilijikita katika makubaliano kimataifa kuhusu usalama, wahamiaji wa mpango na wa mara kwa mara uliopangwa kukamilika mwaka 2018.

Bwana Swing amesema kongamano hilo lililofanyika mara tu baada ya mkutano wa Umoja wa Mataif a wa wakimbizi na wahamiaji mwezi Septemba mjini New York umekuwa mzuri na wa mafanikio.

Ameongeza kuwa kongamano hilo limeweka msingo na maandalizi mazuri wakati dunia ikielekea katika utekelezaji wa makubbaliano hayo ya kimataifa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter