Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA:Mkutano dhidi ya wadudu waharibifu waanza

IAEA:Mkutano dhidi ya wadudu waharibifu waanza

Shirika la kimataifa la nguvu za atomiki IAEA ni mwenyeji wa mkutano wa wataalam wiki hii huko Amerika ya Kusini na Caribbean unaojadili jitihada zinazofanywa kupambana na wadudu au funza waharibifu na tishio kwa mifugo. Tangu mwaka 1970 kumekuwa na kampeni ya mafanikio ili kutokomeza kupitia miundo ya kinyuklia katika baadhi ya nchi.

Kuna nchi kumi na moja zinazohudhuria mkutano huo ulioanza Jumatatu Desemba 12 na utakaoendelea hadi tarehe desemba 16, na kuandaliwa kwa ushirikiano na shirika la chakula na kilimo FAO. Wataalam wanatumia mbinu ya kuwaasi kutozaliana wadudu hao “Sterile Insect Technique"ambayo lengo lake ni kuwadhibiti. Nchi ambazo tayari zimeshiriki katika mradi huo wa miaka mitatu ni: Argentina, Brazil, Chile, Ecuador, Haiti, Panama, Paraguay, Peru na Uruguay. Nchi ya Cuba ambako wadudu hao wapo kwa sasa na Marekani katika jimbo la Florida pia watashiriki kwenye mkutano huo unaofanyika Vienna Austria. Kabla ya kutokomezwa baadhi ya nchi zilipata hasara za kiuchumi zinazokadiriwa kuwa zaidi ya dola bilioni 1.5 kwa mwaka katika eneo hilo. Wadudu hao wanapatikana katika nchi nyingi za Amerika ya Kusini na nchi tano za Caribbean. Msimamizi wa idara ya FAO na IAEA wa mbinu za nyuklia kwa chakula na kilimo Walther Enkerlin amesema jitihada zinaendelea za kulinda maeneo yasiyokuwa na wadudu hao  na kudhibiti kwingineko katika nchi wanachama.