Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi wa afya Aleppo na machungu kwa maisha yao

Wafanyakazi wa afya Aleppo na machungu kwa maisha yao

Ghasia zikizidi kuendelea nchini Syria, raia na wahudumu wa afya wamearifiwa kulipa gharama kubwa ya zahma hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO Aleppo hii leo ni mji hatari zaidi duniani na maelfu ya watu wasio na hatia wanawake na watoto wameuawa au kujeruhiwa na mamilioni kukimbia makwao wakihofia usalama.

Hata hivyo WHO imesema wafanyakazi wa afya pamoja na hatari, nao wanashuhudia zaidi machungu ikitolea mfano muuguzi mmoja ambaye katika kuhudumia wagonjwa alishuhudia maiti ya ndugu yake.

Mwakilishi wa WHO nchini Syria Elizabeth Hoff amesema hajawahi kushuhudia madhila kama hayo tangu kuanza kazi yake.

Amesma wanachofanya sasa ni kuwapatia wauguzi mafunzo ya kisaikolojia ili kuhimili mazingira wanayokumbana nayo.