Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa mtandaoni waanzishwa kufuatialia lengo la afya kwa wote

Mfumo wa mtandaoni waanzishwa kufuatialia lengo la afya kwa wote

Shirika la afya duniani, WHO limeanzisha mfumo mpya mtandaoni unaolenga kufuatilia lengo la kuhakikisha huduma ya afya inapatikana kwa kila mtu ulimwenguni ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni sehemu ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Uzinduzi wa mfumo huo unaenda sambamba na siku ya WHO ya upatikanaji wa huduma ya afya kwa wote hii leo wakati huu ambapo takribani watu milioni 400 duniani hawana uhakika na huduma  muhimu za afya.

Kwa mantiki hiyo mfumo huo wa mtandaoni unaweka huduma muhimu za afya kuanzia uendelezaji wa huduma za kinga, matibabu, huduma za uangalizi baada ya matibabu na hata huduma kwa wale walio taabani.