Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yahitaji dola milioni 70 kukwamua wenye utapiamlo Yemen

UNICEF yahitaji dola milioni 70 kukwamua wenye utapiamlo Yemen

[caption id="attachment_304021" align="alignleft" width="350"]dailynews246b-16

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema kwa mwaka ujao 2017 litahitaji dola milioni 70 ili kukabiliana na utapiamlo nchini Yemen.

UNICEF imesema mahitaji hayo yanalenga kusaidia watoto wanaokabiliwa na utapiamlo, na maeneo yaliyoathirika zaidi ni Hodeida, Sa’ada, Taizz, Hajjah na Lahej is huku Sa’ada likiwa ni jimbo linaloongoza duniani kwa kuwa na watoto wadumavu.

Mohammed Al Asaadi ni Afisa wa Unicef kutoka Yemen.

(SAUTI YAMohammed Al-Asaadi, )

"Utapia mlo ni moja ya changamoto sugu inayoikiabili Yemeni kwa miongo , lakini hali zimezidi kuwa mbaya kutokana na vita hivi vilivyoshika kasi 2015.Kuna watoto zaidi ya milioni 2.2 nchini yemen , na takriban 460,000 wana unyafuzi”

UNICEF imesema hata kabla ya mzozo, utapiamlo ulikuwa umekithiri Yemen kutokana na umaskini na ukosefu wa uhakika wa chakula na sasa hali ni mbaya kutokana na huduma za afya kusambaratika.

Hivyo UNICEF imetaka pande kwenye mzozo Yemen kuwezesha watoa huduma kufikisha misaada hiyo yenye lengo la kuboresha lishe.