Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atuma salamu za rambirambi Uturuki

Ban atuma salamu za rambirambi Uturuki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea Jumamosi katika mji mkuu wa Uturuki, Istanbul na kukatili maisha ya makumi ya watu huku yakijeruhi wengine wengi.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo, Ban amesema anatumai kwamba wahusika wa kitendo hicho cha kigaidi watatambuliwa haraka iwezekanavyo na kufikishwa mbele ya sheria.

Ban pia ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga, watu na serikali ya Uturuki na kuwatakia ahueni majeruhi.