Rais Jammeh aheshimu uchaguzi wa watu kwa amani-UM

11 Disemba 2016
Baraza la Usalama leo limeelani vikali kitendo cha Rais wa Gambia Yahya Jammeh cha kukanusha matokeo ya uchaguzi wa hivi karibuni nchini humo.
Wanachama 15 wa baraza hilo wametoa wito kwa Rais Yahya kutekeleza mchakato wa mpito kwa amani na utaratibu na kuheshimu chaguo la watu huru wa Gambia, kama alivyofanya siku ya Disemba pili, na kuhamisha bila ya vikwazo na kwa haraka madaraka hayo kwa Rais mteule, Mheshimiwa Adama Barrow.
Baraza pia limetoa wito kwa pande zote kujizuia na uhasama na kuhakikisha kikamilifu usalama wa rais mteule Barrow na wa raia wa Gambia.
Vile vile Baraza limeitaka Umoja wa Kiuchumi wa Afrika Magharibi (ECOWAS) kuhakikisha usalama wa ukanda wa Afrika ya Magharibi na nafasi kwa serikali iliyochaguliwa kutawala kwa amani.
Baraza hilo limewapongeza wananchi wa Gambia kwa kufanya uchaguzi uliowazi na wenye amani.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter