Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa Afrika wawajibike ili intaneti inapatikane kwa watu wao: Nsokolo

Viongozi wa Afrika wawajibike ili intaneti inapatikane kwa watu wao: Nsokolo

Kongamano la tisa la kimataifa kuhusu utawala wa mtandao limekamilika huko Mexico ambako pamoja na azimio la kuongeza fursa za mtandao wa intaneti duniani, usawa wa kijinsia mtandaoni umesisitizwa.

Taarifa ya kukamilika kwa mkutano huo ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa, imesema kuna pengo kubwa kati ya wanawake na wanaume katika matumizi ya mtandao huo na kuongeza kuwa ikiwa pengo hilo litazibwa, wanawake watanufaika na matumizi ya mtandao wa intaneti.

Katika mahojiano na Jorge Miyares wa redio ya Umoja wa Mataifa, Deogratius Nsokolo Rais wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania aliyehudhuria kongamano hilo amesema changamoto kubwa inayokabili nchi za Afrika ni kuweka mazingira kwa intaneti kufikia makundi mengi zaidi.

(Sauti ya Nsokolo)

Ameeleza hali ya matumizi ya intaneti barani Afrika hususani Tanzania.

( Sauti ya Nsokolo)

Kisha akasema jukumu la wahudhuriaji katika mkutano huo.

( Sauti ya Nsokolo)