Usalama wa watu Aleppo bado uko njia panda

Usalama wa watu Aleppo bado uko njia panda

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema bado inatiwa hofu na usalama wa raia Aleppo Syria, na hasa waliosalia katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi n ahata wale waliokimbia maeneo yanayodhibitiwa na serikali.

Ofisi hiyo inasema inaamini kuna takribani raia laki moja Mashariki mwa Aleppo kunakodhibitiwa na waasi na watu wengine 30,000 wanaaminika kuwa katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali na watu 500 wanahitaji huduma ya haraka ya afya.

Rupert Colville msemahi wa ofisi ya haki za binadamu anaongeza  kuwa raia wanatumika kama rehani na wanazuiliwa kuondoka katika ukiukaji mkubwa wa kuchukua hatua za kuhakikisha raia wanalindwa kutokana na athari za mashambulizi.

Amesema uhalifu wa vita wa kuchukua watu mateka kuna uwezekano umetendeka.