Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna uhusiano baina ya uhalifu wa mazingira na shughuli zingine haramu:UNEP

Kuna uhusiano baina ya uhalifu wa mazingira na shughuli zingine haramu:UNEP

Ripoti mpya ya shirika la kimataifa la polisi INTERPOL na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira (UNEP) inahusisha uhalifu wa mazingira na shughuli zingine haramu ikiwemo ufisadi, bidhaa bandia, biashara haramu ya ya mihadarati, uhalifu wa mtandao,  uhalifu wa kifedha ikiwa ni pamoja na mashirika ya kigaidi na makundi ya waasi yenye silaha.

Uhalifu wa mazingira kwa mujibu wa ripoti hiyo ni wa kimataifa na ulio mbaya zaidi, kwani unazipokonya serikali rasilimali zinazohitajika kukusanya mapato, unapora watu maisha yao, na kuzinyima jamii amani na usalama .

Ripoti hiyo inasema jumuiya ya kimataifa inahitaji kuunga mkono mtazamo wa kina kukabiliana na uhalifu huo kwa kufuatilia sera kwa vitendo hasa kuhakikisha utekelezaji wake na uchukuaji wa sheria. Ripoti hiyo ya pamoja :mazingira, amani na usalama :viko katika tisho ilitolewa wiki hii katika wiki ya sheria, haki na maendeleo 2016 iliyofadhiliwa na Benki ya dunia.

Utafiti umefanyika katika nchi karibu 70 na kubaini kwamba zaidi ya asilimia 80 ya nchi wanalichukulia uhalifu wa mazingira kama kipaumbele cha taifa na wengi wanaamini kwamnba ongezeko la shughuli za kihalifu ni tishio kubwa kwa amani na usalama duniani.