Skip to main content

Muziki wa asili Ma'di hatarini kutoweka Uganda

Muziki wa asili Ma'di hatarini kutoweka Uganda

Muziki na Ngoma ya "Ma’di-Bowl" au bakuli huchezwa na jamii ya Ma'di nchini Uganda kwa hafla mbalimbali, ikiwa ni pamoja na harusi na kusherehekea mavuno, kwa ajili ya kuimarisha uhusiano wa familia na kujifunza kuhusu utamaduni wa jamii, na pia kuihimarisha mila.   Wazee na viongozi wamejaribu kuziweka na kupitisha mila hizi kwa vijana, lakini kuna tahadhari ya kupotea maana vijana wanafikiri zimepitwa na wakati.

Shirika la  Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, linahimiza makabila mbalimbali waweze kuenzi na kutunza utamaduni wao.  Ungana na Amina Hassan kwa undani wa makala hii