Neno la wiki: FILA
Wiki hii tunaangazia neno "Fila" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.
Neno Fila ina maana mbili, ya kwanza neno hili hutumika katika msemo kwa maana ya "Ubaya" kwa mfano Lila na Fila haitangamani kumaanisha wema na ubaya havisikilizani, pili, Fila ni kifaa kinachotumiwa kujazia wino kwenye mashine ya chapa.